Pages

Ads 468x60px

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

Sample text

Sample Text

Featured Posts

Thursday, October 24, 2013

Polisi waonya waandishi Kenya

Picha za magaidi walioteka jengo la Westgate
Wakuu wa idara ya Polisi nchini Kenya wamewaonya waandisi wa habari kuhusu walivyoripoti matukio katika jumba la Westgate ambako magaidi walishambulia zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Onyo hili linakuja baada ya taarifa za wanajeshi kufanya uporaji katika jengo hilo wakati wakipambana na magaidi hao waliokuwa wamewateka nyara watu waliokuweme ndani ya jumba hilo.
Mkuu wa polisi, David Kimaiyo alisema kuwa waandishi hawapaswi kutoa kuchochea Propaganda, au kuwachochea wakenya wakati wakipeperusha matangazo yao.
Duru zinasema kuwa baadhi ya waandishi wa habari wamehojiwa na polisi hii leo.
Picha za CCTV zilizofichuliwa kwa waandishi wa habari zilionyesha wanajeshi wakitoka ndani ya jumba hilo na mifuko ya plastiki zilizoshukiwa kuwa na bidhaa kutoka katika mojawapo ya maduka makubwa yaliyokuwa ndani ya jengo hilo la Nakumatt.
Hata hivyo jeshi limekanusha madai hayo na kusema kuwa wanajeshi walikuwa wanachukua maji ya kunywa wakati wa operesheni yao dhidi ya magaidi.
Takriban watu 67 walifariki ikiwemo wanajeshi na mamia ya wengine kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo liliosababishwa na Al Shabaab kama walivyokiri. Waliwateka nyara watu ndani ya jingo hilo kwa siku nne.
Pamoja na kupora, vyomo vya habari Kenya vimesema kuwa baadhi ya wanajeshi waliuwana na wenzao wakati wa operesheni yao kutoka na kile kilichosemekana kuwa ukosefu wa maelekezo mazuri kuoka kwa wakuu wa usalama.

Monday, October 21, 2013

Je wanajeshi wa Kenya walipora Westgate?


Mmoja wa wanamgambo wa Al Shabaab wanaosemekana kuuawa kwa shambulizi la Westgate
Picha za wanajeshi wa Kenya waliokwenda katika jumba la Westgate katika juhudi za uokozi na kisha baadaye kuonekena kwenye kamera za CCTV wakiondoka na mifuko ya plasitiki yenye bidhaa za madukani, bila shaka zimewashangaza wengi.
Picha hizo mwanzo zimeonyesha wanajeshi wakiingia ndani ya jengo hilo wakiwa wamebeba silaha kukabiliana na wanamgambo walioshambulia jengo hilo wiki nne zilizopita na baadaye wakitoka wakiwa wamebeba mifuko hiyo wakiwa na silaha zao kwa wakati mmoja.
Hata hivyo haijulikani walichokuwa wamekibeba kwenye mifuko hiyo .
Pamoja na picha za wanajeshi wakiwa wamebeba mifuko, pia kulikuwa na picha zengine zilizoonyesha mashine ya pesa zikiwa zimeporwa ndani ya mikahawa huku picha za alama za risasi kwenye maeneo ya kuhifadhia pesa, pia zikionekana.
Inaarifiwa ilikuwa jaribio ya kufungua hifadhi hizo ambalo halikufanikiwa.
Madai haya ya wanajeshi kufanya uporaji wa maduka katika jingo hilo, yalikanushwa vikali na jeshi la Kenya kiasi cha kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya waliokuwa wanatoa madai hayo, lakini haijulikani jibu lao litakuwa nini hasa kwa picha hizo za CCTV zilizoonyesha wanajeshi hao wakifanya uporaji.
Wamiliki wa maduka waliorejea kwenye maduka yao bbaada ya shambulizi , walidai kuwa maduka yao yaliporwa ingawa jeshi lilikanusha madai hayo baadhi ya taarifa zikisema kuwa ilikuwa njama ya wafanyabiashara kudai fidia kwa mali zao zilizoharibika.
Sio wanajeshi pekee waliotuhumiwa kwa uporaji, kwani polisi mmoja naye alifikishwa mahakamani kwa kosa la uporaji baada ya kupatikana na pochi la mtu liliokuwa na damu.
Wangambao wa Al Shabaab waliteka nyara jengo la Westgate kwa siku nne na kusababisha vifo vya watu 60 pamoja na kuwajeruhi zaidi ya watu miamoja.

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

You can also receive Free Email Updates:

Powered By Blogger Widgets